MWANAFUNZI WA MWAKA WA TATU Bsc. AEA SUA .NAISHIYE OLE LONING'O ANG'ARA KATIKA MASHINDANO YA IBUA UNIVERSITY DEBATE

IBUA ni Taasisi inayoshirikiana na Financial Sector Deepening Trust(FSDT) kuibua sauti za vijana wadogo (16-24) katika sector ya Fedha katika uchumi wa nchi yetu.
 
Tar 16 November ,2019,kulikuwa na "UNIVERSITY DEBATE" Katika Mkoa wa Morogoro ukiwa na kichwa cha mdahalo "Je,Vijana wa kike na kiume wakishiriki katika huduma za kifedha ,itasaidia kukuza uchumi wa nchi yetu?" Ikiwa imechagua mwakilishi mmoja katika kila chuo cha Morogoro(SUA,Mzumbe,St.Joseph na MUM) kuwa wakilishi.
 
Na katika mdahalo huo Naishiye E. Ole Loning'o Mwaka wa 3 katika Shahada ya Uchumi na Kilimo aliwakilisha Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA) na Kuibuka kuwa mshindi wa pili katika mashindano hayo yaliyofanyika Katika Chuo Kikuu Cha Mzumbe,Tarehe 16 Novemba ,2019.
 
 

naishie4

 

naishie2

naishie3naishie5