ZOEZI LA UHAKIKI

Wanajumuiya wa Shule ya Uchumi Kilimo na Stadi za biashara mnakumbushwa kuwa zoezi la uhakiki kwa kutumia kitambulisho cha Taifa kwa wafanyakazi wa shule litafanyika tarehe 05/07/2017 katika ukumbi wa mikutano wa BALAZA la chuo jengo la utawala kuanzia saa 2:00 asubuhi mpaka saa 11:00 jioni. Kwa wasiokuwepo kwa sababu mbalimbali wanaweza kuhakikiwa tarehe 12 na 13/07/2017 kuanzia saa 2:00 mpaka 11:00 jioni. Kwa wafanyakazi waliopo masomoni nje ya nchi, Mkuu wa Idara husika ya mfanyakazi huyo atapaswa kuwasiliana nae na kisha nyaraka tajwa ziwasilishwe kwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Utawala na fedha) kwa uhakiki. Wakati wa zoezi la uhakiki unatakiwa kuwa na i) Hati ya malipo ya hivi karibuni (salary slip), ii) Kitambulisho cha kazi, iii) Kitambulisho cha Taifa au namba ya Kitambulisho cha Taifa. Kila la Kheri. 

OUR ADRESS

Dean, School of Agricultural Economics and Business Studies,
P.O. Box 3007,
CHUO KIKUU SOKOINE,
MOROGORO.
Tel: +255 (0) 23 2603415
E-mail: daea@suanet.ac.tz

FOLLOW US

VISITORS

We have 13 guests and no members online